Header Ads

IJUE SARATANI YA MATEZI YA MATE NA ZAKE TIBA


Https://mbochiherbal.blogspot.com
E-mail Address;
Mbochiherballife646@gmail.com

Mpendwa msomaji wangu ninakusalimu kwa jina lipitalo majina yote,furaha yangu katika mada hii tuambatane pamoja kugundua nini chanzo na zake tiba kwa ugonjwa huu hatari
 Binadamu ameumbwa akiwa na matezi makubwa matatu ya mate,Yaliyoko kila upande wa uso,kwa maana hiyo kila mtu ana jumla ya matezi makubwa 6 ya mate
     Ni matezi haya ndiyo ambayo huzalisha mate na kwa kupitia mirija maalumu,mate hayo huweza kuingia kinywani na kufanya kazi ipaswayo na mate kinywani,mojawapo ya kazi kubwa ya mate kinywani ni kuwa kilainishi cha kinywa.pamoja na kuwa na jumla ya matezi makubwa 6 ya mate kinywani,pia kinywani kuna mamia ya matezi madogo ya kuzalisha mate ambayo kwa kufanya kazi na matezi makubwa,huwezi kufanya kinywa chako kuwa na afya ya kawaida

SARATANI YA MATEZI YA MATE HUANZAJE
Saratani ya matezi ya mate ambayo inaanzia hasa kwenye matezi ya mate,ni moja ya saratani chache kutokea ukilinganisha na saratani zinazotokea kwenye sehemu nyingine za kinywa
    Saratani ya matezi ya mate inaweza kuanza kwenye tezi lolote la mate kinywani,hata hivyo tezi ambalo huwa linashambuliwa zaidi ni tezi kubwa zaidi liitwalo Parotid,tezi hili liko mbele kidogo ya sikio lako la kila upande

DALILI ZA SARATANI YA TEZI LA MATE
   Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na uvimbe karibuni na taya ama shingoni au kinywani,pia hali ya kupooza kidogo sehemu ya usoni ya upande ulioathirika,ni moja ya dalili za saratani hiyo na muathirika anaweza kubaini hali ya kudhoofika kwa misuli ya upande Wa uso ulioathiriwa
    Pia kuwa na maumivu yasiyo koma kwenye eneo la tezi husika pamoja na kupata shida wakati Wa kufungua kinywa kwa uwazi

NI WAKATI GANI UMUONE DAKTARI

Wataalamu Wa afya wanashauri mgonjwa anapaswa kumuona daktari Mara tu anapobaini dalili zilizotajwa hapo,Ili uchunguzi ufanyike mapema
   Hata hivyo kuwa na uvimbe katika maeneo ya matezi ya mate ama jirani nayo inaweza kusababishwa na vitu vingi ikiwamo maambukizi ya matezi (Infection) ama mawe kwenye matezi ya mate (Salivary gland stone)

SABABU YA MTU KUUGUA SARATANI  HII
   Kitaalamu bado haijajulikana husababishwa na mini,Ingawa kuna sababu kadhaa ambazo zinaaminika zinaweza kuchangia MTU kupata saratani ya tezi la mate

SABABU HATARISHI ZINAZOWEZA KUEPUKWA
  Umri mkubwa,unadaiwa huweza kuwa chanzo ingawa saratani hii inaweza kutokea katika umri wowote,Mara nyingi huwa inagundulika kwa watu wazima

Maoni 2 :

  1. Je kuna tiba ya uhakika juu ya maradhi hospital na mgonjwa akapona kabisa. Na je katika tiba asili pia untibika?

    JibuFuta
  2. Naomba ushauri wa tiba Nina tatizo la uvimbe nyuma ya masikio pia nahisi maumivu ya taya na candidias kwenye ulimi na koo.

    JibuFuta

Inaendeshwa na Blogger.