Header Ads

UPUNGUFU WA KINGA MWILINI NDIYO CHANZO KIKUU CHA MAGONJWA MENGI NYEMELEZI (CD4)



 CD4 NI NINI?
maana ya cd4  ni cluster differentiation 4 (Immunity)
Http//mbochiherbal.blogspot.com
Address
Mbochiherballife646@gmail.com
Call bye using phone number
+2550757349219

MADA YA LEO NI UPUNGUFU WA KINGA MWILINI
kwa ufupi mpendwa Wa mbochi herbal neno Ukimwi ni kifupisho cha kiingereza AIDS, ni ugonjwa unaotokana na virus ambavyo uitwa VVU ni virus vya ukimwi,kwa kiingereza tunasema HIV (human immunodeficiency virus) na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maradhi nyemelezi
Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya binadamu kwa kuwa husababisha vifo kwa walio wengi na hatimae watu utengwa
Ukimwi umekuwa na madhara makubwa katika jamii na kuhusu ukimwi kama vile unaweza kuambukizwa kwa kugusana nae bila ngono,ugonjwa huu pia unasababisha madhara ya kiuchumi

UPUNGUFU maana yake (ukimwi) unaharibu uwezo wa kupambana na ugonjwa,si ukimwi moja kwa moja unaoweza kuua lakini mashambulio ya magonjwa ambayo kwa kawaida yasingekuwa tatizo kubwa

1.Kinga inahusu mfumo wa kingamwili ambazo ni uwezo wa mwili kujitetea dhidi ya ugonjwa
2.Mwili usio na kinga ya kutosha unapatwa na matatizo mbali mbali kwa sababu mfumo wa kinga umeharibika na hauwezi kupigana na ugonjwa wowote

Aids maana yake ni nini.?
AIDS-Acquired immunology deficiency syndrome
*ACQUIRED-maana yake mtu awezi kuwa na hali hii kiasili ameipata
*IMMUNE- Hii inataja ya kwamba tatizo linahusu Immune system yani mfumo wa kingamwili
*Deficiency-Inamaanisha ya kwamba kuna kasoro
*SYNDROME-Ni mkusanyiko wa matatizo ya kiafya ili hali kingamwili haufanyi kazi tena,mgonjwa ana athiriwa na magonjwa mbali mbali na kuonyesha dalili za magonjwa hayo yote

MFUMO WA KINGAMWILI NA VVU

Kila MTU huwa na mfumo Wa kingamwili ndani yake,seli za ulinzi zinazunguka mwili na kutafuta vidubini vya nje vinavyoweza kuleta mvurugo na zinaviharibu,kati ya seli hizi za ulinzi ni seli nyeupe za damu (Lukosaiti) ambayo ni muimu sana

Ukimwi unasababishwa na VVU,kama virus vyote,vvu vinaingia katika mwili kwa kusudi la kuzaa,virus haviwezi kuzaa peke yake vinahitaji seli pindi vinapoweza kuingia ndani ya seli na kutumia mfumo wa seli kwa kunakili DNA yake

Kwa kawaida virus vinashambuliwa na mfumo wa kingamwili na kuharibika,lakini VVU vina tabia mbili za pekee ambazo zinavifanya mwili kuwa katika hatari
*VVU uwa vinafahulu mara nyingi kuepukana na seli za ulinzi mwilini
*Vinaingia hasa hasa katika seli nyeupe za damu

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.